-
Maandalizi-
-
Kupika-
-
Walaji1
Sosi ya ukwaju (Tamarind Paste), ni sosi yenye mchanganyiko wa ladha ya utamu na uchachu, ambayo hutengenezwa kwa kutumia ukwaju na maji. Sosi hii hutumika kuongeza ladha kwenye vyakula vya aina mbalimbali, kama vile nyama, saladi, wali, mboga, n.k. Fuata hatua zufuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza sosi hii ya ukwaju.
Ingredients
Directions
Chukua kikombe 1 cha maji, kisha roweka ukwaju ndani ya hicho kikombe chenye maji kwa muda wa saa 1 hadi saa 2.
Sugua ukwaju huo kwa kutumia vidole vya mikono yako ili kuondoa mbegu zake, kisha tupa mbegu hizo.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka mchanganyiko wa ukwaju kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.
Weka ½ kikombe cha maji yaliyobaki, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.
Weka sosi hiyo kwenye chombo safi chenye mfuniko, kisha hifadhi kwenye friji.
Leave a Review