-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 30
-
Walaji4
Sosi ya uyoga na lozi, ni sosi tamu ambayo hupikwa kwa kutumia uyoga, vitunguu maji, mtindi, lozi mbichi, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Sosi hii yafaa kula pamoja na wali, mkate au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika sosi hii ya uyoga na lozi.
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu maji, tangawizi, vitunguu swaumu, lozi, mbegu za mpopi, pamoja na garam masala, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mdalasini pamoja na iliki, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde kadhaa.
Weka mchanhanyiko wa vitunguu maji ulio usaga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona mchanganyiko huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka mbegu za giligilani, kungumanga, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde kadhaa.
Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga. Weka uyoga, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga, kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo ona uyoga umetoa maji maji yake.
Mimina maji halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.
Weka majani ya giligilani, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 2, au hadi utakapo ona yamenyauka.
Weka pilipili manga halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review