-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 45
-
Walaji4
Sosi ya viungo, ni sosi yenye rangi ya machungwa na ladha nzuri ya kuvutia, ambayo hupikwa kwa kutumia, vitunguu maji, nyanya, mtindi, pamoja na viungo. Sosi hii yafaa kula pamoja na wali mweupe, wali wa binzari nyembamba, chapati au mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika sosi hii ya viungo.
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu swaumu, tangawizi, pamoja na vitunguu maji, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena dogo.
Weka nyanya kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa nyanya hizo kwenye mashine ya kusaga na uziweke pembeni kwenye kontena jingine dogo.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka mchanganyiko wa vitunguu maji ulio usaga kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3.
Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha endelea kukaanga mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Ongeza moto na uweke moto wa wastani. Weka nyanya ulizo zisaga, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.
Weka mbegu za giligilani, binzari nyembamba, majani ya uwatu, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda aa dakika 2 mpaka 3.
Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga.
Mimina maji halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review