Jarida la Mapishi

Supu ya choroko na spinachi

Supu ya choroko na spinachi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 45
  • Walaji
    4

Supu ya choroko na spinachi, ni supu tamu iliyo sheheni virutubisho vingi vya Protini, Vitamini A, pamoja na madini ya chuma. Supu hii hupikwa kwa kutumia choroko, spinachi, viazi mviringo, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Supu hii yafaa sana kunywa katika msimu wa baridi pamoja na mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ukifunze jinsi ya kupika supu hii ya choroko na spinachi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, choroko, viazi, maji, tangawizi, vitunguu swaumu, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa kwa muda wa dakika 5.

    Step2

    Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona choroko zimeiva.

    Step3

    Weka spinachi pamoja na majani ya giligilani halafu koroga vizuri, kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5 mpaka 10 zaidi, kisha epua na umimine kwenye kontena.

    Step4

    Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba pamoja na mbegu za giligilani, kisha koroga vizuri. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena lenye supu, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.