-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 40
-
Walaji8
Supu ya kabichi, ni supu tamu na rahisi kupika ambayo hupikwa kwa kutumia kabichi, mboga mchanganyiko, viazi, kitunguu maji, nyanya, limao, pamoja na viungo. Supu hii yafaa kunywa katika msimu wa baridi. Waweza kuipika supu hii katika muda mfupi sana wa ndani ya dakika 40 tu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya kabichi.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.
Weka viazi mviringo, mboga mchanganyiko, kabichi, spinachi, pamoja na nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.
Mimina maji hakafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona mboga zimeiva.
Weka majani ya mvuje, pilipili manga, majani ya giligilani, garam masala, chumvi, majani ya minti, pamoja na limao halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 15 zaidi. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review