-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 30
-
Walaji4
Supu ya karoti, ni supu nzuri iliyo sheheni ladha ya karoti, ambayo hupikwa kwa kutumia karoti, mtindi, vitunguu maji, limao, pamoja na viungo mbalimbali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya karoti.
Ingredients
Directions
Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za pilipili manga kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.
Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu mbegu za pilipili manga ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimesagika vizuri.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, majani ya mbei, binzari nyembamba, pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.
Weka tangawizi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka karoti pamoja na majani ya giligilani, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona karoti zimbadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka vikombe 5 vya maji halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona karoti zimeiva, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe. Ondoa majani ya mbei kwenye sufuria na uyaweke pembeni.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka mchanganyiko wa supu ya karoti kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wa supu umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa supu kwenye mashine kusaga na uirudishe kwenye sufuria.
Rudisha sufurua kwenye jiko, kisha chemsha hadi utakapo ona supu imepungua kwa kiwango cha ¼.
Mimina mtindi halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, weka limao pamoja na pilipili manga halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review