-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 45
-
Walaji3
Supu ya kuku, ni supu tamu yenye viungo ambayo hupikwa kwa kuchemsha nyama ya kuku kwenye maji pamoja na viungo. Supu hii yafaa kula majira ya jioni kabla ya chakula cha jioni, katika kipindi cha msimu wa vuli. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya kuku.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa. Weka ndani ya hilo sufuria, kuku, maji, pilipili manga, chumvi, karafuu, majani ya mbei, mdalasini, vitunguu swaumu, iliki, tangawizi, pamoja na limao, halafu koroga vizuri, kisha weka sufuria hilo kwenye jiko lenye moto mkubwa, halafu acha ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 45, au hadi utakapo ona nyama ya kuku imeiva na kuwa laini.
Epua supu na upakue kwenye bakuli safi, tayari kwa kunywa.
Leave a Review