-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 40
-
Walaji4
Supu ya maboga, nu supu tamu na rahisi kupika. Supu hii hupikwa kwa kutumia maboga, ambayo huchemshwa pamoja na viazi mviringo na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya maboga.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, maboga, viazi mviringo, vitunguu maji, tangawizi, vitunguu swaumu, binzari ya manjano, chumvi, pamoja na vikombe 4 vya maji, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona maboga yameiva na kuwa laini, kisha epua supu na uweke pembeni ili ipoe.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka supu uliyo chemsha kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona imesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa supu hiyo kutoka kwenye mashine ya kusaga na uirudishe kwenye sufuria.
Weka kwenye kwenye hilo sufuria limao pamoja na kikombe 1 cha maji yaliyobaki, harafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa kwa muda wa dakika 2.
Chukua kikaango kidogo chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, black seeds, mbegu za uwatu, binzari nyembamba, pamoja na mbegu za shamari, halafu koroga vizuri. Epua na umimine mchanganyanyiko huu kwenye sufuria lenye supu, kisha koroga vizuri.
Acha supu iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5 zaidi, kisha epua na upakue kwenye chombo safi tayari kwa kula.
Leave a Review