-
MaandaliziDakika 30
-
KupikaDakika 50
-
Walaji4
Supu ya maharage, ni supu tamu na rahisi kupika. Supu hii hupikwa kwa kutumia maharage mekundu, mtindi, nyanya, tomato sauce, pamoja na viungo. Supu hii yafaa sana kunywa jioni pamoja na chakula chochote cha jioni. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya maharage.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria dogo. Weka kwenye hilo sufuria, maharage, maji, pamoja na chumvi, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona maharage yameiva, kisha epua na uweke pembeni.
Chukua sufuria la ukubwa wa wastani lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.
Weka tangawizi, vitunguu swaumu, pamoja na nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.
Wela mbegu za giligilani pamoja na binzari ya manjano, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.
Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 1.
Weka maharage uliyo chemsha, majani ya giligilani, pamoja na tomato sauce, halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 5.
Weka garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review