-
MaandaliziDakika 30
-
KupikaDakika 40
-
Walaji4
Supu ya mbaazi, ni supu tamu na rahisi kupika ambayo yawafaa hasa wale ambao hawapendi kula supu zenye nyama. Supu hii hupikwa kwa kutumia mbaazi, nyanya, sosi ya ukwaju, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya mbaazi.
Ingredients
Directions
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka kikombe 1 cha maji, kisha roweka mbaazi ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.
Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, mbaazi pamoja na maji uliyotumia kurowekea mbaazi, tangawizi, binzari ya manjano, chumvi, pamoja na kikombe 1 cha maji, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu acha iendelee kuchemka huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona mbaazi zimeiva, kisha epua na uweke pembeni.
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, nyanya, Tamarind Paste, pamoja na vikombe 4 vya maji vilivyobaki, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona nyanya zimeiva.
Mimina mchanganyiko wa choroko ulio chemsha kwenye sufuria lenye mchanganyiko wa nyanya halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke.
Ukiona imechemka, epua supu na umimine kwenye kontena.
Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, binzari nyembamba, majani ya mvuje, pamoja na majani ya giligilani, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena lenye supu, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.
Leave a Review