Jarida la Mapishi

Supu ya mboga

Supu ya mboga | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 25
  • Walaji
    4

Supu ya mboga, ni supu tamu ambayo hupikwa kwa kutumia mchanganyiko wa mboga mbalimbali kama vile; kiazisukari chekundu, viazi mviringo, tanipu na karoti. Supu hii yafaa kula pamoja na tambi, chapati, mkate au sandwich. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya mboga.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, kiazisukari chekundu, viazi mviringo, tanipu, karoti, vitunguu maji, nyanya, tangawizi, majani ya giligilani, pamoja na vikombe 3 vya maji, halafu funika sufuria, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa kwa muda wa dakika 1.

    Step2

    Punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step3

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka mchanganyiko ulio uchemsha kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na urudishe kwenye sufuria ulilolitumia kuchemshia.

    Step4

    Weka kikombe 1 cha maji yaliyobaki kwenye hilo sufuria, kisha koroga vizuri.

    Step5

    Rudisha sufuria hilo kwenye jiko lenye moto mkubwa. Weka chumvi, pilipili manga, pamoja na limao, halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke.

    Step6

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5, kisha epua na uweke pembeni kwenye kontena.

    Step7

    Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za kisibiti, pamoja na garam masala, kisha changanya vizuri. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena lenye supu, kisha koroga vizuri, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.