-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 15
-
Walaji4
Supu ya mtindi, ni supu nzuri na rahisi kupika ambayo yaweza kunywewa katika misimu ya vipindi vyoye vya mwaka. Supu hii husaidia kuongeza joto mwilini katika majira ya baridi. Waweza kunywa supu hii pamoja na chakula chochote ukipendacho. Fuata hatua zifuatazo, ili ukifunze jinsi ya kupika supu hii ya mtindi.
Ingredients
Directions
Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka kwenye hicho kikaango, mchele mweupe, choroko, adesi, pamoja na mbegu za binzari nyembamba, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 3, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga mchanganyiko wa mchele ulio ukaanga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena.
Weka kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, mtindi, maji, tangawizi, pamoja na vitunguu swaumu, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Weka binzari ya manjano, chumvi, pamoja na mchanganyiko wa mchele ulio usaga mwanzoni, kisha saga tena hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri na kuwa laini.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, majani ya mvuje, pamoja na mchanganyiko wa mtindi ulio usaga, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke huku ukikoroga mara kwa mara.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10.
Weka majani ya giligilani halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review