-
MaandaliziDakika 30
-
KupikaDakika 50
-
Walaji4
Supu ya nazi, ni supu nzuri ambayo hupikwa kwa kutumia tui la nazi pamoja na nazi iliyokunwa. Ukiachana na nazi, supu hii huwekewa viungo vya aina mbalimbali kama vile; binzari nyembamba, mbegu za haradali, n.k, ambavyo huifanya supu hii iwe tamu na yenye ladha ya kipekee zaidi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya nazi.
Ingredients
Directions
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka vikombe 2 vya maji, kisha roweka mbaazi ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, mbaazi pamoja na maji uliyotumia kurowekea mbaazi, binzari ya manjano, chumvi, pamoja na kikombe 1 cha maji, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu acha iendelee kuchemka huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona mbaazi zimeiva, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka mchanganyiko wa mbaazi ulio chemsha kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona mbaazi hizo zimesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huu kwenye mashine ya kusaga na urudishe kwenye sufuria.
Chukua sufuria jingine kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, binzari nyembamba, pilipili manga, majani ya mvuje, pamoja na nazi iliyokunwa, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.
Weka Tamarind Paste pamoja na vikombe 2 vya maji vilivyobaki, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona nyanya zimeiva na kuwa laini.
Mimina mchanganyiko wa mbaazi ulio chemsha, halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 5.
Weka tui la nazi pamoja na majani ya giligilani halafu koroga vizuri, kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 2 zaidi. Epua na upakue kwenye chombo safi tayari kwa kula.
Leave a Review