-
Maandalizi-
-
KupikaSaa 1
-
Walaji3
Supu ya nyama, ni pishi tamu, lenye virutubisho vingi na rahisi kupika, ambayo unaweza kupika kwa kutumia nyama yoyote ile uipendayo, iwe ni nyama ya ng’ombe, nyama ya mbuzi, au nyama ya kondoo. Fuata hatua zifuatazo, ili kujifunza jinsi ya kupika supu hii ya nyama.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, nyama, majani ya giligilani, pilipili hoho, vitunguu maji, pilipili manga, chumvi, karafuu, majani ya mbei, karoti, tanipu, mbegu za giligilani, mdalasini, vitunguu swaumu, iliki, maji, pamoja na tangawizi, halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa saa 1, au hadi utakapo ona nyama imeiva, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review