Jarida la Mapishi

Supu ya nyanya na choroko

Supu ya nyanya na choroko | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 45
  • Walaji
    4

Supu ya nyanya na choroko, ni supu tamu ambayo yafaa kunywa katika kipindi cha baridi, hasa kutokana na choroko kuwa na protini kwa wingi, ambayo husaidia kuongeza joto mwilini. Supu hii hupikwa kwa kutumia nyanya, choroko, kitunguu maji, kiazi mviringo, karoti, maharage machanga, pamoja na viungo vy aina mbalimbali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya nyanya na choroko.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, tangawizi, majani ya giligilani, choroko, vitunguu swaumu, vitunguu maji, viazi mviringo, pilipili manga, chumvi, nyanya, karoti, maji, pamoja na maharage machanga, halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

    Step2

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 35, au hadi utakapo ona choroko na viazi vimeiva, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step3

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga mchanganyiko ulio uchemsha, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huu kwenye mashine ya kusaga na urudishe kwenye sufuria.

    Step4

    Weka sufuria hilo kwenye jiko lenye moto mkubwa, kisha acha ichemke.

    Step5

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 7 mpaka 10. Epua supu na umimine pembeni kwenye kontena, kisha funika vizuri kontena hilo.

    Step6

    Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za giligilani pamoja na mbegu za binzari nyembamba, kisha koroga vizuri. Epua na umimine kwenye kontena lenye supu, kisha koroga vizuri, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.