-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 35
-
Walaji6
Supu ya nyanya na mboga, ni supu tamu ambayo hutengengenezwa kwa kutumia, nyanya, mboga mchanganyiko, vitunguu maji, liki, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Waweza kula supu hii yenyewe kama ilivyo, au pamoja na chakula chochote kile ukipendacho. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya nyanya na mboga.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, jani la mbei, binzari nyembamba, pamoja na liki, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 4, au hadi utakapo ona liki imeanza kubadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka vitunguu swaumu, tangawizi, pamoja na mashina ya figili, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.
Weka mbegu za giligilani, kisha koroga vizuri.
Weka mboga mchanganyiko, halafu kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona zimeiva, kisha epua na uweke pembeni kwenye kontena.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, nyanya pamoja na majani ya giligilani, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke kwenye sufuria ulilolitumia kupika mboga mchanganyiko.
Weka chumvi pamoja na pilipili manga, kisha koroga vizuri.
Rudisha sufuria kwenye jiko lenye moto mkubwa, kisha acha ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo. Mimina maji halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10.
Weka mboga mchanganyiko ulizopika mwanzoni halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 5. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review