-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 15
-
Walaji4
Supu ya uyoga, ni supu tamu na yenye afya, ambayo hupikwa kwa kutumia uyoga mweupe au uyoga wa kahawia, mtindi, maziwa, pamoja na viungo. Upishi wa supu ya uyoga unahitaji sana uvumilivu ili uweze kupata ladha nzuri kwenye supu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya uyoga.
Ingredients
Directions
Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka kwenye hicho kikaango, mbegu za pilipili manga pamoja na mbegu za binzari nyembamba halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.
Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu, mbegu za pilipili manga pamoja na mbegu za binzari nyembamba ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimesagika vizuri.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka liki kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka uyoga pamoja na vitunguu swaumu, halafu pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona uyoga umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mchanganyiko wa uyoga ulio upika, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, mtindi, maziwa, mchanganyiko wa uyoga ulio usaga, limao, mchanganyiko wa pilipili manga ulio utwanga, pamoja chumvi, kisha koroga vizuri. Funika kontena hilo vizuri, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 2, kabla ya kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review