Jarida la Mapishi

Tanipu zenye binzari ya manjano

Tanipu zenye binzari ya manjano | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 20
  • Walaji
    4

Tanipu zenye binzari ya manjano, ni mboga rahisi kupika ambayo hupikwa kwa kutumia tanipu, vitunguu maji, binzari ya manjano, pamoja na viungo vingine. Mboga hii yafaa kula pamoja na chapati au nyama ya kuchoma hasa nyama ya kuku. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika tanipu hizi zenye binzari ya manjano.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka tangawizi kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step2

    Weka binzari nyembamba pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 5, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

    Step3

    Weka tanipu, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 4.

    Step4

    Punguza moto na uweke moto mdogo. Weka sukari halafu funika sufuria, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7.

    Step5

    Weka majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.

    Step6

    Nyunyizia garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.