-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 20
-
Walaji4
Tosti ya kifaransa, ni kitafunio cha kifungua kinywa kinacho tengenezwa kwa kutumia slesi za mikate, mayai, maziwa, pamoja na viungo. Unaweza kupika tosti hii ya kifaransa kwa muda mfupi sana wa ndani ya dakika 10 tu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza tosti hii ya kifaransa.
Ingredients
Directions
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka ndani ya hilo kontena, mayai, mtindi, majani ya giligilani, pamoja na chumvi, kisha piga piga mchanganyiko huo vizuri.
Chukua kikaango cha ukubwa wa wastani chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto.
Chukua slesi moja ya mkate. Laza upande wa kwanza wa slesi hiyo, kwenye mchanganyiko wa mayai na ukandamize taratibu, hadi utakapo ona mchanganyiko huo umeenea vyema kwenye upande huo wa kwanza wa slesi. Geuza slesi upande wa pili, kisha ilaze kwenye mchanganyiko wa mayai na ukandamize taratibu, hadi utakapo ona mchanganyiko huo umeenea vyema kwenye upande huo wa pili wa slesi.
Weka slesi kwenye kikaango, kisha kaanga kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona upande wa kwanza wa slesi hiyo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Geuza slesi upande wa pili, kisha kaanga kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona upande wa pili wa slesi hiyo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa slesi hiyo kwenye kikaango na uiweke pembeni kwenye chombo safi, tayari kwa kula. Rudia hatua ya 3 na ya 4 kwa slesi zilizobaki.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review