-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 15
-
Walaji4
Viazi vitamu vya kuchemsha, ni chakula kizuri chenye afya kilicho sheheni virutubisho vingi hasa Wanga, Vitamini A, Vitamini C, pamoja na Vitamini B6. Viazi hivi hupikwa kwa kuvichemsha pamoja na ukwaju na viungo. Viungo vinavyowekwa katika viazi hivi husaidia kuongeza ladha na kuvifanya viazi hivi viwe vitamu zaidi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika viazi hivi vitamu vya kuchemsha.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, viazi vitamu, maji, pamoja na chumvi, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa kwa muda wa dakika 1 mpaka 2.
Punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona viazi vimeiva.
Weka Tamarind Paste pamoja na Chaat Masala, kisha pika mchanganyiko huo huku ukivigeuza viazi mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3, au hadi utakapo ona maji yote kwenye sufuria yamekauka.
Weka majani ya giligilani, halafu pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review