Jarida la Mapishi

Viazi vyenye binzari nyembamba

Viazi vyenye binzari nyembamba | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 35
  • Walaji
    4

Viazi vyenye binzari nyembamba, ni chakula ambacho hupikwa kwa kutumia viazi mviringo, limao, pamoja na viungo vya aina mbalimbali, kama vile binzari nyembamba. Viazi hivi vyafaa kula pamoja na wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika viazi hivi vyenye binzari nyembamba.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vimeiva.

    Step2

    Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.

    Step3

    Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.

    Step4

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za giligilani, chumvi, pamoja na viazi mviringo, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona viazi vimemebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step5

    Weka limao pamoja na majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.

    Step6

    Nyunyizia pilipili manga halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.