Jarida la Mapishi

Viazi vyenye karanga

Viazi vyenye karanga | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 45
  • Walaji
    4

Viazi vyenye karanga, ni chakula kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kutumia viazi mviringo, karanga, limao, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Viazi hivi vyafaa kula kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi, au kama kitafunio cha kawaida wakati wowote. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika viazi hivi vyenye karanga.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vimeiva.

    Step2

    Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.

    Step3

    Menya maganda ya viazi hivyo, halafu vikate katika vipande vidogo vidogo, kisha viponde nusu ya viazi hivyo.

    Step4

    Chukua kikaango kikubwa chenye siagi pamoja na mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha siagi na mafuta vipate moto. Weka kwenye hicho kikaango, karanga pamoja na tangawizi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step5

    Weka viazi mviringo pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona viazi vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step6

    Weka majani ya giligilani pamoja na limao, kisha koroga vizuri.

    Step7

    Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha pika mchanganyiko huo bila kukoroga kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona upande wa chini umetengeneza ukoko wa rangi ya kahawia.

    Step8

    Geuza upande wa pili wa mchanganyiko huo, halafu pika na upande huo wa pili bila kukoroga kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona upande wa chini umetengeneza ukoko wa rangi ya kahawia, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.