Jarida la Mapishi

Viazi vyenye pilipili hoho

Viazi vyenye pilipili hoho | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 30
  • Walaji
    4

Viazi vyenye pilipili hoho, ni chakula kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia mviringo vilivyo chemshwa, pilipili hoho, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Chakula hiki chafaa kula chenyewe kama kilivyo, au waweza kula pamoja na wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika viazi hivi vyenye pilipili hoho.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vimeiva.

    Step2

    Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.

    Step3

    Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.

    Step4

    Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia pamoja na siagi na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha siagi na mafuta vipate moto. Weka kwenye hicho kikaango, binzari nyembamba, pilipili manga, majani ya uwatu, mango powder, mbegu za giligilani, chumvi, pamoja na viazi mviringo, kisha kaanga huku ukivigeuza viazi mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo ona viazi vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step5

    Weka majani ya giligilani pamoja na pilipili hoho halafu funika kikaango, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5.

    Step6

    Nyunyizia garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.