Jarida la Mapishi

Viazi vyenye vitunguu na nyanya

Viazi vyenye vitunguu na nyanya | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 45
  • Walaji
    4

Viazi vyenye vitunguu na nyanya, ni chakula kizuri kilicho sheheni wanga, ambacho hupikwa kwa kutumia viazi mviringo vilivyo chemshwa, kitunguu, nyanya, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika viazi hivi vyenye vitunguu na nyanya.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vimeiva.

    Step2

    Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.

    Step3

    Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.

    Step4

    Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona vimeiva.

    Step5

    Weka nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 4, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.

    Step6

    Weka binzari ya manjano, binzari nyembamba, mbegu za giligilani, pamoja na chumvi, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step7

    Weka viazi mviringo ulivyo vichemsha pamoja na majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona viazi mviringo vimechanganyika vyema pamoja na vitunguu maji na nyanya.

    Step8

    Nyunyizia garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.