Jarida la Mapishi

Vimanda vya ukwaju

Vimanda vya ukwaju | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 10
  • Walaji
    4

Vimanda vya ukwaju, ni kitafunio kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia mayai, vitunguu maji, vitunguu vya kijani, pilipili hoho, ukwaju, pamoja na viungo. Vimanda hivi vyafaa kula kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi pamoja na chai au kahawa. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika vimanda hivi vya ukwaju.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka ndani ya hilo kontena, mayai, majani ya giligilani, pilipili hoho, pilipili manga, chumvi, vitunguu swaumu, Tamarind Paste, tangawizi, sukari, pamoja na vitunguu vya kijani, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

    Step3

    Weka mchanganyiko wa mayai uliochanganya, kisha funika kikaango na ukaange kwa muda wa dakika 4, au hadi utakapo ona upande wa chini wa mchanganyiko huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. (Weka mchanganyiko huo wa mayai kwa awamu 2)

    Step4

    Chukua sahani kubwa. Weka sahani hiyo ndani ya kikaango, kisha pindua kikaango juu chini ili kimanda kipate kigeuka na kuhamia kwenye sahani.

    Step5

    Telezesha kimanda kwenye kikaango, halafu rudisha kikaango kwenye jiko, kisha kaanga upande wa pili wa kimanda hicho kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona na upande huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step6

    Kunja kimanda katikati, kisha ondoa kwenye kikaango na ukiweke kwenye sahani, tayari kwa kula. Rudia hatua ya 3 mpaka 6, kwa mchanganyiko wa vimanda uliobaki.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.