Jarida la Mapishi

Viungo vya chai

Viungo vya chai | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    -
  • Walaji
    1

Viungo vya chai, ni mchanganyiko wa viungo vya aina mbalimbali, ambavyo hutumika kuongeza ladha kwenye chai na kuifanya chai hiyo iwe tamu zaidi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza viungo hivi vya chai kwa ajili ya kuuza, au kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mbegu za shamari, mbegu za iliki, majani ya minti, pamoja na mbegu za pilipili manga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri.

    Step2

    Weka tangawizi, mdalasini, pamoja na karafuu, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.

    Step3

    Weka viungo hivyo kwenye chombo safi chenye mfuniko, kisha hifadhi mahali pakavu penye baridi.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Recipe Reviews

    • Malaika

      Woooow!!!! Asante Kwa bandiko!!!

    • Modest Mugeyo

      mbegu za shamari jina lingine zinaitwaje

      • Mary Joachim

        Mbegu za shamari, kwa jina jingine huitwa fennel seeds. Ukienda kwenye maduka ya viungo ya Wahindi, huwezi kuzikosa kwa jina hili.

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.