-
MaandaliziDakika 30
-
KupikaDakika 15
-
Walaji4
Wali mweupe, ni chakula maarufu na kinacholiwa zaidi kuliko chakula cha aina yoyote duniani, ambacho hupikwa kwa kutumia, mchele, maji, pamoja na chumvi. Karibu nusu ya watu wote waliopo duniani, wanakula wali. Unaweza kupika wali huu kwa kutumia njia ya kuchemsha (boiling method), au kwa kutumia njia ya mvuke (steam method) ambayo ndio inayotumika kwenye pishi hili. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika wali huu mweupe.
Ingredients
Directions
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.
Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, mchele, maji uliyotumia kurowekea mchele, pamoja na chumvi, halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.
Zima jiko, kisha acha wali utulie kwa muda wa dakika 5, ukiwa bado juu ya jiko. Baada ya dakika 5, pakua wali kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review