Jarida la Mapishi

Wali wa kukaanga wa kamba

Wali wa kukaanga wa kamba | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 20
  • Kupika
    Dakika 10
  • Walaji
    4

Wali wa kukaanga wa kamba, ni chakula kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia kamba wabichi, mboga, wali mweupe uliopikwa, soy sauce, pamoja na viungo. Chakula hiki chenye utamu wa kipekee, kitakufanya uache kabisa kununua wali wa kukaanga wa kwenye hoteli. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika wali huu wa kukaanga wa kamba.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango kikubwa chenye vijiko 2 vya chai vya mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kamba kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3. Ondoa kamba hao kwenye kikaango na uwaweke pembeni kwenye sahani.

    Step2

    Weka vijiko 2 vya chai cha mafuta ya kupikia kwenye kikaango hicho hicho, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu vya kijani, tangawizi, uyoga, mboga ya figili, pamoja na karoti, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3.

    Step3

    Chukua bakuli. Weka ndani ya hilo bakuli, ute wa mayai 2 pamoja yai 1 zima, halafu piga piga mayai hayo vizuri, kisha mimina kwenye kikaango na uache yaive upande wa chini kwa muda wa sekunde 10 mpaka 20.

    Step4

    Weka maharage pamoja na wali mweupe, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1 mpaka 3.

    Step5

    Weka njegere, soy sauce, pamoja na kamba ulio kaanga, halafu changanya vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.