-
MaandaliziDakika 30
-
KupikaDakika 15
-
Walaji4
Wali wa kukaanga wa nyama ya nguruwe, ni chakula kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia wali, nanasi, nyama ya nguruwe tangawizi, karoti pamoja na majani ya figili. Mchanganyiko wa mahitaji haya hufanya chakula hiki kiwe cha kuvutia na chenye ladha nzuri. Ikiwa wewe ni mpenzi wa wali wa kukaanga, basi nakuhakikishia utakipenda chakula hiki. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika wali huu wa kukaanga wa nyama ya nguruwe.
Ingredients
Directions
Chukua kikaango kikubwa chenye vijiko 2 vya chai vya mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka nyama ya nguruwe kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 4 mpaka 5. Ondoa nyama hiyo ya nguruwe kwenye kikaango na uiweke pembeni kwenye sahani.
Weka kijiko 1 cha chakula cha mafuta ya kupikia kwenye kikaango hicho hicho, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu vya kijani, vitunguu swaumu, mboga ya figili, tangawizi, karoti, pamoja na vipande vya nanasi, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 4 mpaka 5.
Chukua bakuli. Weka ndani ya hilo bakuli, ute wa mayai 2 pamoja yai 1 zima, halafu piga piga mayai hayo vizuri, kisha mimina kwenye kikaango na uache yaive upande wa chini.
Chukua bakuli. Weka ndani ya hilo bakuli, ute wa mayai 2 pamoja yai 1 zima, halafu piga piga mayai hayo vizuri, kisha mimina kwenye kikaango na uache yaive upande wa chini.
Weka wali mweupe, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1 mpaka 2.
Weka nyama ya nguruwe uliyo ikaanga, njegere, soy sauce, pamoja na majani ya giligilani, halafu changanya vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review