-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 20
-
Walaji4
Wali wa mtindi, ni chakula kikuu na maarufu sana ambacho hupikwa kwa kutumia wali uliochanganywa pamoja na mtindi na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika wali huu wa mtindi.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, mchele pamoja na maji, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka, kisha epua na uweke pembeni. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.
Chukua kikaango cha ukubwa wa wastani chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, vitunguu maji pamoja na tangawizi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka wali ulio upika pamoja na chumvi, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona wali umechanganyika vyema pamoja na vitunguu maji na tangawizi.
Weka mtindi pamoja na majani ya giligilani halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review