Jarida la Mapishi

Zucchini zenye nazi

Zucchini zenye nazi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 15
  • Walaji
    4

Zucchini zenye nazi, ni mboga tamu na rahisi kupika, ambayo hupikwa kwa kutumia zucchini zilizo katwa katwa, nazi, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mboga hii yafaa kula pamoja na wali, mkate au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mboga hii ya zucchini zenye nazi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, tangawizi, vitunguu swaumu, majani ya mvuje, majani ya giligilani, pamoja na nazi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step2

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka mchanganyiko wa tangawizi ulio usaga kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step3

    Weka mbegu za giligilani, binzari ya manjano, chumvi, pamoja na zucchini, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3.

    Step4

    Mimina tui la nazi halafu funika sufuria, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona zucchini zimeiva. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.