-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 40
-
Walaji4
Supu ya maboga, nu supu tamu na rahisi kupika, ambayo hupikwa kwa kutumia maboga, viazi mviringo, vitunguu maji, limao, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Supu hii yafaa kula pamoja na chapati au mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya maboga.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, maboga, viazi mviringo, vitunguu maji, tangawizi, vitunguu swaumu, binzari ya manjano, chumvi, pamoja na vikombe 4 vya maji, halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona vimeiva, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, supu uliyo ipika, kisha saga hadi utakapo ona supu hiyo imesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa supu hiyo kwenye mashine ya kusaga na urudishe kwenye sufuria, kisha weka sufuria hilo kwenye jiko lenye moto wa wastani.
Weka limao kwenye hilo sufuria, kisha koroga vizuri.
Mimina vikombe 2 vya maji halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke kwa muda wa dakika 2.
Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, black seeds, mbegu za uwatu, binzari nyembamba, pamoja na mbegu za shamari, kisha koroga vizuri. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye sufuria lenye supu, kisha koroga vizuri.
Acha supu ichemke kwa muda wa dakika 5 zaidi, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review