-
MaandaliziDakika 30
-
KupikaDakika 30
-
Walaji4
Ingredients
Directions
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.
Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kipate moto. Weka njugu za pistachio kwenye hicho kikaango, halafu kaanga huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, kisha epua na uweke pembeni.
Chukua bakuli ndogo. Weka maziwa, kisha roweka zafarani ndani ya hilo bakuli lenye maziwa kwa muda wa dakika 15.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, tangawizi, binzari nyembamba, iliki, pamoja na pilipili manga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka mchele, maji uliyotumia kurowekea mchele, pamoja na chumvi, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona wali umekaribia kuiva.
Funua sufuria na unyunyizie juu ya huo wali maziwa yenye zafarani, kisha funika tena sufuria na uendelee kupika huo wali kwa muda wa dakika 5 zaidi. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.
Wali ukishaiva zima jiko na uache utulie kwa muda wa dakika 5, ukiwa bado juu ya jiko. Nyunyizia garam masala, lozi, pamoja na njugu za pistachio halafu koroga vizuri, kisha pakua pilau kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review