Jarida la Mapishi

Achari ya minti na maembe

Achari ya minti na maembe | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 10
  • Walaji
    1

Achari ya minti na maembe, ni achari nzuri na maarufu, ambayo hutengenezwa kwa kutumia majani ya minti, maembe, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Achari hii yafaa kutumika kwenye vitafunio, kama vile sambusa. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza achari hii ya minti na maembe.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za binzari nyembamba kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step2

    Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu mbegu za binzari nyembamba ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimesagika vizuri.

    Step3

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, tangawizi iliyo twangwa, majani ya minti, pamoja na ½ kikombe cha maji, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step4

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, sukari pamoja na vikombe 3 vya maji, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 4, au hadi utakapo ona sukari yote imeyeyuka.

    Step5

    Weka mchanganyiko wa tangawizi ulio usaga, maembe, Chaat Masala, tangawizi ya unga, binzari nyembamba, chumvi, pamoja na black salt, halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke.

    Step6

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha acha iendelee kuchemka huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step7

    Weka achari hiyo kwenye chombo safi chenye mfuniko, kisha hifadhi kwenye friji.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.