-
MaandaliziSaa 1 Dk. 30
-
KupikaDakika 25
-
Walaji4
Pilau ya uyoga na pistachio, ni pilau tamu na rahisi kupika, ambayo hupikwa kwa kutumia uyoga ulio kaushwa, mchele, njugu za pistachio, pamoja na viungo. Pilau hii yafaa kuliwa kama chakula cha mchana au cha jioni, pamoja na saladi ya vitunguu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya uyoga na pistachio.
Ingredients
Directions
Suuza vizuri uyoga huo kwenye maji yanayo tiririka.
Chukua kontena. Weka maji, kisha roweka uyoga ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa saa 1. Baada saa 1, mwaga maji yote yaliyomo kwenye kontena na kubakiwa na uyoga peke yake.
Osha uyoga huo kwenye maji yanayo tiririka, kisha ukate kate katika vipande vidogo vidogo.
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mdalasini, iliki, majani ya mbei, pamoja na pilipili manga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka binzari nyembamba pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5.
Weka tangawizi, vitunguu swaumu pamoja na majani ya minti, kisha endelea kukaanga.
Weka mchele pamoja na maji uliyotumia kurowekea mchele, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka, lakini wali bado haujaiva.
Weka uyoga, majani ya giligilani, pamoja na pistachio halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uendelee kupika wali huo kwa muda wa dakika 5 mpaka 7 zaidi, au hadi utakapo ona wali umeiva.
Wali ukishaiva zima jiko na uache utulie kwa muda wa dakika 5, ukiwa bado juu ya jiko. Baada ya dakika 5, pakua pilau kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review